SHINDANO LA SERENGETI MASTA LAWASHA MOTO ULAYA ULAYA BAR YA MANZESE - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

SHINDANO LA SERENGETI MASTA LAWASHA MOTO ULAYA ULAYA BAR YA MANZESE

Mkazi wa Manzese jijini Dar es salaam Joachim Mwale (kushoto) akishiriki  kwenye droo ya kumtafuta “Serengeti Masta” wa baa ya Ulaya Ulaya iliyopo Manzese jijini Dar es salaam wakati promosheni hiyo ilipofunga kambi ndani ya baa hiyo mwishoni mwa wiki. (Kulia) ni Mshereheshaji wa shindano hilo Masta Razani Kapalatu. 
Mshereheshaji wa shindano la Serengeti Premium Lager liliopewa jina la “Serengeti Masta” Razani Kapalatu akiwa pamoja na mabalozi wa bia ya Serengeti premium Lager ambao kwa pamoja walitoa maelezo kwa wateja wa bia hiyo waliofika kushiriki katika shindano la kumtafuta Serengeti Masta ndani ya baa ya Ulaya Ulaya iliyopo Manzese jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Shindano hilo limedumu jijini Dar na mikoani kwa takriban muda wa miezi miwili sasa na kuweza kuzifikia baa mbalimbali ambapo zawadi mbalimbali kama fedha taslim, fulana na bia za bure zimekuwa zikitolewa katika kuwahamasisha wateja wa bia hiyo kuendelea kuwa pamoja.
Mshereheshaji wa shindano la Serengeti Masta Razani Kapalatu( akionyesha kiasi cha Tsh. 50,000/= alichomkabidhi mshindi wa shindano la Serengeti Masta ambaye aliitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager wakati wa promosheni hiyo iliyofanyika katika baa ya Ulaya Ulaya iliyopo Manzese jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni mteja aliyeibuka “Serengeti Masta” wa baa hiyo ambaye alifahamika kwa jina la Doris Frances.
Mshindi wa shindano la Serengeti Masta Doris Frances (kushoto) kwenye picha ya pamoja na marafiki zake mara baada ya kuibuka bingwa wa kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti na kukabidhiwa zawadi ya Tsh 50,000 wakati wa promosheni hiyo iliyofanyika mwishoni wa wiki katika baa ya Ulaya Ulaya iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.
Mshereheshaji wa shindano la Serengeti Masta Razani Kapalatu akitoa zawadi ya fulana kwa mkazi wa Manzese na mpenzi wa bia ya Serengeti Premium Lager Rodgers Robert wakati wa promosheni ya kumtafuta Serengeti Masta iliyofanyika katika baa ya Ulaya Ulaya ya Manzese jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya bia ya Serengeti Premium Lager imezifikia baa zaidi ya mia tano kwa mikoa minne ambayo ni Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya na kufanikiwa kutoa elimu juu ya bia hiyo na ubora wake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.