Shilole kuchora tattoo nyingine ya Nuh Mziwanda kalioni! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole kuchora tattoo nyingine ya Nuh Mziwanda kalioni!

Hivi karibuni Zuwena Mohamed ‘Shilole’ alichora tattoo yenye jina la boyfriend wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kwenye kifua chake, ikiwa ni ishara ya kuwa mapenzi yao yanazidi kushamiri.
shilole-2
Kama vile haitoshi Shishi bado ana mpango wa kuongeza mchoro mwingine kwenye sehemu za siri.
Akizungumza na Global Publishers, Staa huyo wa mduara, Shishi amesema ana mpango wa kuchora tena jina la mpenzi wake, Nuh kwenye moja ya kalio lake ikiwa ni njia mojawapo ya kuonyesha mapenzi yake ya dhati kwake.
shilole-1
“Mimi bado tattoo moja ya muhimu sana ambayo nataka kuchora kwenye kalio ili kuonyesha ni jinsi gani nampenda mpenzi wangu Nuh,” alisema Shilole.
Nuh Mziwanda ndiye aliyekuwa wa kwanza kuchora tattoo zenye majina ya Shilole kwenye mwili wake, kitendo kilichomshawishi mpenzi wake Shishi naye kuchora.

Source: GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.