Roma atangaza kuachia wimbo mpya October 25 siku ya uchaguzi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Roma atangaza kuachia wimbo mpya October 25 siku ya uchaguzi

Baada ya kukumbana na changamoto nyingi alipoachia wimbo wake wa ‘Viva Roma Viva’, Rapper wa Tongwe Records, Roma ametangaza kuja na wimbo mpya ambao atauachia siku ya uchaguzi mkuu.
roma new pic
October 25 siku ambayo Watanzania watajipanga kwenye mistari kwajili ya kushiriki zoezi muhimu la kuwachagua viongozi wanaowataka, rapper Roma amepanga kuwapa wimbo mpya utakaotoka siku hiyo.
Roma ambaye amekutana na vikwazo vingi kupitia wimbo huu wa sasa VRV ikiwemo BASATA kutangaza kuufungia, ametumia mitandao ya kijamii kuwataarifu mashabiki kuhusu ujio wa wimbo mpya ambao hajasema utaitwaje.
“#ON_SET Guess what!!!!!!! MY NEW SONG loading….. Nitai#RELEASE On 25th OCTOBER” aliandika Roma.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.