Penny na Siza Wanaswa Kimahaba, Ipo hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Penny na Siza Wanaswa Kimahaba, Ipo hapa

WATANGAZAJI wa Shindano la Bongo Star Search, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Siza Daniel wamenaswa wakioneshana mahaba hadharani kama mtu na ‘bebi’ wake.
Tukio hilo lililopigwa chabo na paparazi wetu lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Kawe Beach, Dar wakati wawili hao walipokuwa wakijiandaa kurekodi kipindi cha shindano hilo ambapo walionekana kushea juisi ambayo kuna wakati Siza alimnywesha Penny huku wakati mwingine, Penny akijibu mapigo.
Wawili hao baada ya kupigwa picha na paparazi wetu na kuwauliza kama ni wapenzi, Siza alishindwa kuzungumza lolote lakini Penny alipoulizwa kama jamaa huyo ndiye mrithi wa Diamond (Nasibu Abdul), alijibu kwa kifupi:
“Jamani kusoma hujui hata picha huoni?”

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.