INAWEZEKANA KUSHARE PICHA KWENYE MITANDAO KUKAANZA KUA KUGUMU. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

INAWEZEKANA KUSHARE PICHA KWENYE MITANDAO KUKAANZA KUA KUGUMU.

Bet Sasa


INAWEZEKANA KUSHARE PICHA KWENYE MITANDAO KUKAANZA KUA KUGUMU. 
Na John Conor, Bongoswaggz.
 
Kushare picha inaweza kuanza kua ngumu.
  Wiki hii, shirika linaloweka viwango vya tehema kwa ajili ya mfumo wa JPEG unaotengeneza picha, Umeanza kufikiria kutambulisha DRM(Digital Right Management) software, ambayo inazua watu kuiga(copy) au kusambaza file lolote linalotumia mfumo wa JPEG.

Picha nyingi unazoziona kwenye mitandao ya internet zimetengenezwa kwa mfumo wa JPEG au JPG. Hatua hii inaweza kukuzuia kusambaza au kuweka kwenye mitandao kama facebook picha yeyote yenye mfumo huo ambayo haujaitengeneza mwenye au haujapata kibali cha kuisambaza.

Hiyo itakua ni pigo kubwa kwa tamaduni ya kusambaza(share) ambayo imekua ndiyo msingi wa internet kwa zaidi ya muongo mmoja sasa. Makundi ya kutetea haki za kidigitali za watumiaji wa internet, yameanza kujiandaa na mapambano dhidi ya software hii.

 DRM(Digital Right Management) ni nini?
 Sasa ivi, hakuna kinachomzuia mtu yeyote kuiga mara nyingi kadri awezavyo file lolote kwenye internet. Inawezekana ikawa ni kinyume cha sheria kuchapisha kwa mara nyingine picha ya mpiga picha fulani kwenye tovuti yako, ila hakuna kinachokuzuia kitehama kufanya hivyo.
Lakini kuna software iliopo inayoweza kuzuia uchapishaji usio na kikomo wa mafile. Inaitwa DRM kifupi cha (Digital Right Management). Inazoelekea kupatikana kwenye file za muziki. Kama umeshawahi kukumbana na error message inayosema huwezi kucheza file hili la sauti(audio), hiyo ndiyo DRM.

Picha zinaweza ziwaka zinafuta.
Kamati ya Joint Photographics Expert Group (JPEG), Kikundi kilichopo nyuma ya JPEG kinasema inampango wa kutengeza kiwango kinachotambua usambazaji wa taarifa za picha salama, chenye uwezo wa kuhakikisha ubinafsi(privacy), uhifadhi wa taarifa bila kubadilishwa(data integrity) na kuhakisha haki ya umiliki wa taarifa.
Wiki hii kamati hiyo ilikaa 'Brussels' kwa madhumuni ya kujadili swala hili.

Kama mfumo huu ungeanza kutumika kwa wingi. Ingekua na maana kua usingeweza kuiga(copy)picha utakayo kutana nayo kwenye tovuti ya habari, au kudownload picha ya rafiki yako wa facebook aliyoiweka kwenye mtandao huo. Hii ingekua ni pigo takatifu kwa tamaduni iliyozoeleka kwenye internet ya kusambaza(share) picha.

Pia software hii inadhumuni la kuongeza ubinafsi wa mtuamiaji. Kamati hiyo inasema, uwezekano wa upatikanaji na utumiaji rahisi wa picha katika internet, umeleta ongezeko la matatizo ya uchapishaji usiotarajiwa wa taarifa binafsi. Kwa mfano picha zilizochapishwa kwenye mtandao wa facebook kwa ajili ya watu wachache kuziona, ila zikavuja na kuonekana na hadhira.

Kwa hiyo DRM itakua na uwezo wa kuzuia watu flani wasio na ruhusa maalumu kupata au kuona baadhi ya picha.

Bado hakuna mda maalumu uliotegwa.
 Msemaji wa kamati ya JPEG Dr Touradj Ebrahimi ameliambia shirika la BBC kua mabadiliko yeyote yanaweza kua chaguo(opt-in). DRM haiwezi kua katika picha zako kama hautaki iwepo. "Kitu kimoja mnatakiwa muelewe ni kua hatulazimishi mfumo huu, ila tunasema acha watu wawe na changuo. Wale wanaoona mfumo wa hivi sasa uko vizuri kabisa na mwanataka kua na picha ambazo hazina ulinzi [wanaweza kufanya hivyo]. "

Pia alisema "bado hakuna mpango wa uhakika wa kubadilisha mfumo wa JPEG, ila matumaini ya kutafuta majawabu ya technologia pale ambapo vipengele vya mpango huu mpya vitaamuliwa" BBC inaripoti.
Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.