Nay Wa Mitego Uso Kwa Uso Na Majambazi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay Wa Mitego Uso Kwa Uso Na Majambazi

Msanii wa muziki Nchini Tanzania, Emmanuel Elibariki "Ney wa Mitego"
Nay wa Mitego
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Nay wa Mitego amevamiwa na majambazi nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana.
Tukio hilo limetokea wakati Nay wa Mitego akiwa mkoani kwa ajili ya harakati za kampeni za kisiasa na lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Nay amesema kuwa majambazi hao waliokuwa wamevalia mask usoni walivamia nyumbani hapo usiku wa manane na kujaribu kukata nyaya za security Alarm wakashindwa ndipo wakaamua kupanda kwenye nguzo ya umeme kwa lengo la kukata umeme nyumba nzima.
Zoezi hilo nalo lilishindikana baada ya majirani kupiga kelele zilizosababisha majambazi hao kutokomea kusikojulikana wakiwa na gari yao aina ya Land Cruiser Nyeusi.
Aidha Nay wa Mitego ameshangazwa na tukio hilo kwani amesema kuwa hana bifu na mtu yeyote mjini lakini anashukuru Mungu kwani familia yake ipo salama na anawashukuru majirani kwa ushirikiano waliouonesha.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.