Mrema ‘Amtosa’ Mgombea Urais TLP, Ampigia Kampeni Magufuli - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mrema ‘Amtosa’ Mgombea Urais TLP, Ampigia Kampeni Magufuli

Bet Sasa
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Mwenyekiti wa TLP taifa, Augustino Mrema leo amemnadi mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kuwa ndiye anafaa kuwa rais wakati chama chake kikiwa kimemsimamisha, Macmillian Lyimo kuwania nafasi hiyo ya urais kwa tiketi ya TLP.
Hali hiyo ilianza kwa Dk Magufuli kumpigia debe Mrema anayewania ubunge Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP kwa kusema kuwa ana historia nzuri na uzoefu katika uongozi kuliko wengine.
Dk. Magufuli alisema hayo hiyo jana wakati akihutubia wananchi katika Uwanja wa Polisi Himo ambapo alisema wananchi wasikosee kwenye kupiga kura na kuwa hata kama hawaitaki CCM, basi wampigie kura Mrema.
“Kama humtaki mgombea wa CCM wa jimbo hilo, Innocent Shirima angalau mniletee Mrema,” alisema Dk Magufuli na kuongeza hata msahau Mrema bali atamtafutia kazi nyingine.
Dk Magufuli aliongeza kuwa kama wananchi wa Vunjo hawatamchagua Shirima au Mrema watapata shida kwani aliwaita wagombea wengine kuwa ni wababaishaji.
Akiomba kura kwa wananchi katika mkutano huo, Shirima mwenyewe alisema endapo atachaguliwa atahakikisha kero ya barabara za Kilema, Mua, Himo, Saidingi, Kahe na Chekereni zinatengenezwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.