Mgombea Ubunge CCM Aanguka Jukwaani Akiruka Kichurachura..Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mgombea Ubunge CCM Aanguka Jukwaani Akiruka Kichurachura..Ipo Hapa

Mgombea ubunge wa tiketi  ya  Chama  Cha  Mapinduzi (CCM) katika  jimbo  la  Tunduru  Kaskazini,Mhandisi Ramo Makani alianguka jukwaani  wakati  akijaribu  kuruka  kichura chura.
Tukio  hilo  lilitokea  katika  mkutano  wa  ufunguzi  wa  kampeni  za  mgombea  huyo, uliofanyika  kwenye  viwanja  vya  baraza  la  Idd  mjini  hapa.
Inasadikiwa  kuwa  alikusudia  kunogesha  staili  ya  mgombea  urais  wa  tiketi  ya  CCM,Dr. John Magufuli  ya  kupiga  Push Up..
Ingawa  tukio  hilo  lilionekana  kumfedhehesha,mgombea  huyo  alijikakamua  kuinuka  huku  akisaidiwa  na  walinzi  wake  na  kuendelea  kunadai  sera  zake.
Alisema  kuwa  katika  kipindi  kilichopita  alitekeleza  ilani  ya  chama  chake  kwa  kusimamia ujuenzi  wa  barabara  ya  Namtumbo-Tunduru  hadi  wilayani Nanyumbu  inayoendelea  kujengwa  kwa  kiwango  cha  lami.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.