MBOWE AFICHUA NJAMA CHAFU ZA CCM KUIBA KURA USIKU WA TAREHE 24 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MBOWE AFICHUA NJAMA CHAFU ZA CCM KUIBA KURA USIKU WA TAREHE 24

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema wamegundua njama za kuiba kura zitakazofanywa na CCM usiku wa tarehe 24 kwa kupita mitaani na kugawa fedha za kura feki.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe vilivyopo jijini Mbeya. 
Alisema ili kudhibiti hali hiyo, siku hiyo Ukawa watafanya doria usiku kucha ili kuhakikisha hakuna fedha zinazogawiwa wala kura feki zitakazosambazwa.
“Nia ya Ukawa ya kupigania Katiba ya wananchi iko pale pale kwani Serikali ya awamu ya tano itaipigania kadri itakavyowezekana ili kiu ya wananchi juu ya Katiba hiyo ipatikane,” alisema Mbowe.
Alisema pia kwamba, uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwa kuwa unahusu maisha ya watu, watoto na utajibu maombi ya Watanzania.
Pamoja na hayo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), siyo huru na kwamba wanachama wa Chadema watahakikisha wanalinda kura zao.
“Kwa miaka 25 tumepiga kelele tukidai tume huru ya uchaguzi lakini kilio chetu hakikusikika kwa sababu CCM inajua tukiwa na tume huru, haiwezi kubaki madarakani.
“Kama tume yetu siyo huru, tuna wajibu wa ziada wa kulinda kura zetu. sheria inasema huturuhusiwi kusimama wala kukaa chini ya mita 200 kutoka kituoni. Kwa hiyo, ukihesabu mita 200 kutoka kituoni, una uhuru wa kuwa eneo hilo,
“Jambo hili limezua hofu ndani ya tume, ndani ya Serikali, ndani ya CCM na kwa Rais Jakaya Kikwete kwa sababu anasema tukishapiga kura, tukalale. Sasa namwambia Rais Kikwete ushauri huo akawape CCM, sisi hatuutaki,” alisema Mbowe.
Alisema pia kwamba, wanachama wa Chadema na wapenzi wao, hawatafanya fujo bali watakuwa na ujasiri wa kupiga na kulinda kura zao kwa sababu hakuna anayeweza kuzuia mpango wa Mungu kwa kutumia askari au nguvu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.