Mastaa 5 Bongo Wenye Vipaji, Lakini Tatizo Nyota - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mastaa 5 Bongo Wenye Vipaji, Lakini Tatizo Nyota

KATIKA ulimwengu wa muziki Bongo, tumekuwa tukiwasikia wasanii wachache wakivuma ndani na nje ya nchi huku wakifanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchi tofauti na Tanzania. Pamoja na hao wachache kuvuma kimataifa, siyo kwamba wanajua sana kuliko wengine ila nyota zao ndizo zinazowasaidia kujikuta wakitajwa kila kona huku wengine wakiwa wanafanya vizuri lakini hawapati bahati hiyo ya kuwa gumzo ndani na nje, tatizo likiwa ni nyota zao ambapo badala yake wamebaki wakisikika akina Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ali Kiba na wengine wachache. Kwenye makala haya tunakuletea orodha ya mastaa wanaofanya vizuri lakini tatizo ni nyota kwani kazi zao ni nzuri lakini hawaoneshi kuwa gumzo na kupata tuzo za kitaifa na kimataifa kama walivyo hao wengine wachache.

Ben Pol
Bernad Paul ndilo jina alilopewa na wazazi wake. Huyu ni mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva na nyimbo nyingi anazoimba na uimbaji wake ni mzuri lakini imekuwa ni vigumu kutoboa kimataifa pia kwa Bongo tuzo nazo zimekuwa zikimpitia mbali. Ben Pol ametamba na ngoma kali kama Jikubali, Unanichora, Sophia na nyingine nyingi.
Belle 9
Wimbo wa Masogange ndiyo uliomtambulisha kwenye anga la muziki. Abednego Damian ‘Belle 9’ aliutendea haki wimbo huo na nyingine alizowahi kuimba kama Shauri Zao, Listen na nyinginezo lakini ameshindwa kutoboa kimataifa kama walivyo akina Ali Kiba na Diamond wakati ni mwanamuziki mzuri.
Mo Music
Moshi Katemi a.k.a Mo Music ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye amefanya ngoma kali kama Basi Nenda, Simama na Nitazoea. Kiukweli jamaa anajua kuimba na kila anapotoa wimbo unabamba na kuwashika vilivyo mashabiki wake. Mo Music nyota yake imeshindwa kung’aa labda kutokana na kwamba hajaingia moja kwa moja kwenye muziki au la kwani alikuwa masomoni huku akiimba.
mavokoRich Mavoko
Richard Martin ni jamaa aliyebamba na nyimbo kama Pacha Wangu,Labda Niseme, Roho Yangu na Moyo. Ana kipaji lakini amejikuta akififia kadiri siku zinavyosonga mbele.
Mwanamuziki huyu hajawahi kufanya kolabo na msanii wa nje ya Bongo na amewahi kusema kwamba hana mpango wa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa kwa sababu anaamini atatoka mwenyewe.

barnaba11Barnaba
Barnaba Elias ni mwanamuziki mzuri unaweza kusema anamshinda hata Diamond kiuwezo kwani amefanya kazi kadhaa zikakubalika. Kwanza ni mtunzi wa nyimbo mbalimbali za wasanii wenzake na za kwake mwenyewe. Pili anajua kuimba na tatu anajua kutumia vyombo vya muziki tofauti na wanamuziki wengi ambao wanajua kuimba tu.
Barnaba amefanya vizuri kwa nyimbo zake kama Suna, Siri aliofanya na Vannesa Mdee, Wahalade ambayo ilipendwa sana na mashabiki wengi na nyingine nyingi ambapo ameshindwa kufika levo za Diamond wakati anastahili hata kumpita.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.