Mashahidi 50 Kutoa Ushahidi Mauaji Ya Bilionea Msuya, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mashahidi 50 Kutoa Ushahidi Mauaji Ya Bilionea Msuya, Ipo Hapa

Bet Sasa


Marehemu Erasto Msuya 
Marehemu Erasto Msuya 
Moshi. 
Tukio la mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa Mererani, Erasto Msuya litawekwa hadharani wiki ijayo wakati mashahidi 50 wa Jamhuri watakapoanza kutoa ushahidi wao kwa siku tano mfululizo.
Mfanyabiashara huyo aliyekuwa akimiliki vitega uchumi kadhaa, aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 12 kwa kutumia bunduki ya SMG Agosti 7,2013 katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai.
Kesi hiyo inayovuta hisia za wakazi wa miji ya Arusha, Moshi na Mererani itasilikizwa mjini Moshi kuanzia Oktoba 5 hadi Oktoba 9 na Jaji Salma Maghimbi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, washitakiwa sita katika kesi hiyo watatetewa na jopo la mawakili watano kutoka mikoa ya Arusha na Dar es Salaam.
Mawakili hao ni Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emanuel Safari na John Lundu wakati upande wa Jamhuri utaongozwa na wakili wa Serikali Mfawidhi,Neema Mwanda akisaidiana na Abdala Chavula.
Februari 10 mwaka huu, Mawakili hao waliiambia mahakama kuwa Jamhuri inakusudia kuita mashahidi 50 kuthibitisha shitaka hilo na kuwasilisha vielelezo 40 ikiwamo bunduki moja ya SMG.

-mwananchi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.