MANENO YA MKE WA WA MAREHEMU MH. DEO FILIKUNJOMBE, YANAUMIZA SANA ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MANENO YA MKE WA WA MAREHEMU MH. DEO FILIKUNJOMBE, YANAUMIZA SANA !


Mjane wa Deo Filikunjombe ametoa ujumbe wenye kugusa Maisha aliyopitia wakati akiwa na mumewe kabla hajafariki. Sarah Filikunjombe amesema hivi:
"Za siku wapendwa nawashukuru wote kwa text nyingi za pole mlizonipa na kuwa pamoja na familia yangu kwa kipindi hiki kigumu kwetu kwa kumpoteza mtu muhimu katika maisha yangu nilizoea kumuita majina mazuri yote ila yale yote ntayahamishia kwa wanangu ulioniachia nawahakikishia nitasimama sehemu zote mbili kama baba na kama mama nitakupenda daima mume wangu deo wangu filikunjombe wangu jembe langu nawashukuru pia wale waliomsema vibaya mume wangu hakika malipo ni hapahapa duniani ni mbaya sana kurukia jambo usilolijua nimekutana na marehemu mwaka 1999 akiwa mwanafunzi wa chuo cha makerere uganda na kufunga nae ndoa 2003 akiwa polisi tulitamani maisha mazuri ila tulishindwa kutokana na ugumu wa maisha tumefanya mambo mengi mpaka kuwa hapa leo ikiwakupiga picha na baadaye tukafungua duka la camera kwa kuanza na kamera tatu tu na juhudi ndio iliomfikasha alipo ishia anaeikashifu nyumba ungejua tulivyoijenga kwa shida usingesema nasema haya kwa maumivu makali sana leo kaiacha hajakaa hata wiki mbili angekuwa na hela siangeijenga zamani leo tungekuwa tumeichakaza ndo akafa naombeni ukiona mtu kapata shida jua namna ya kumfariji sio kuendelea kumumiza asanteni wote by mjane wa filikunjombe"

By Sarahabiba27

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.