Lowassa, Magufuli Kuchunguzwa Mamilioni Ya Kampeni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lowassa, Magufuli Kuchunguzwa Mamilioni Ya Kampeni

Chopa za kampeni zinazotumiwa na wagombea wa CCM pamoja na UKAWA kufanyia kampeni kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Chopa za kampeni zinazotumiwa na wagombea wa CCM pamoja na UKAWA kufanyia kampeni kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania imetoa ufafanuzi madai yanayo enezwa na baadhi ya watu  kuwa wagombea urais wenye upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao ni Edward Lowassa na John Pombe Magufuli huenda wamezidisha gharama za kampeni kutokana na aina ya kampeni wanazo fanya ukilinganisha na vyama vingine.
Kw mujibu wa mwanasheria kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Ludovick Ringia amesema kuwa hakuna uthibitisho utakaoweza kusema kuwa kuna chama kimezidisha gharama mpaka hapo uchaguzi utakapo kamilika.
Amesema   taarifa ya kuzidisha gharama za kampeni kwa baadhi ya vyama ni uvumi kwa kuwa wagombea urais bado hawajamaliza kampeni zao.
Amebainisha kuwa endapo chama au mgombea atakayebainika amepitiliza gharama hizo baada ya uchaguzi sheria itafuata mkondo wake ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashitaka ya kijinai pamoja na kuvuliwa wadhifa wake.
Aidha, amesema sheria zitakazo sababisha mgombea huyo kuzuiliwa ikiwa ni pamoja na kutokujaza fomu au kujaza fomu kwa kudanganya kwa sababu sheria inasema kila chama au mgombea ni lazima aandike gharama zake hata kama vifaa anavyotumia ni vya msaada.
Mwanasheria huyo amesisitiza kuwa sheria ya gharama za chaguzi hazilengi matumizi ya fedha peke yake bali na vifaa kama magari, chopa na vinginevyo lazima vyama viandike ni nani anagharamia na ni kwa kiasi gani gharama za mafuta zinaendesha vyombo hivyo.

-hivisasa

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.