Lil Wayne adai Birdman amewaibia Drake, Nicki Minaj na Tyga mkwanja mrefu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lil Wayne adai Birdman amewaibia Drake, Nicki Minaj na Tyga mkwanja mrefu

Ugomvi kati ya Young Money na Cash Money unaendelea kuwa mkubwa zaidi baada ya Lil Wayne kutoa madai mapya.
birdman-wayne-nicki-drake
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Wayne anadai kuwa na maelezo kutoka kwa wawakilishi wa Drake na Tyga yakisema wameibiwa fedha nyingi.
Kwa upande wa Nicki Minaj, anadai kuwa Young Money imemfanyia uhuni kwa kushindwa kuwalipa maproducer. Young Money inadai kuwa jukumu la kuwalipa watayarishaji lilikuwa la Cash Money.
Young Money imesema inadai fedha kibao kutoka kwenye dola milioni 100 ambazo Cash Money ilipewa na Universal.
Hata hivyo timu ya Birdman imejibu kuwa tayari fedha hizo zimelipwa ambapo dola milioni 20 zilienda kwa Young Money mwaka 2012, milioni 12 zingine zikienda kwenye album ya Lil Wayne na zingine milioni 70 zikilipwa kama advances.
Cash Money wanadai kuwa wasanii wa Wayne walitakiwa watengeneza album 21 lakini wametengeneza 13 tu.
January, Wayne alimshtaki Birdman akimtaka amlipe dola milioni 51.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.