KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI (SBL) YAHITIMISHA KAMPENI YA “SERENGETI MASTA” KWA KISHINDO JIJINI DAR - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI (SBL) YAHITIMISHA KAMPENI YA “SERENGETI MASTA” KWA KISHINDO JIJINI DAR

Msimamizi wa shindano la “Serengeti Masta” Sade Hussein (Kushoto) akitoa maelekezo ya jinsi ya kushiriki kwa washiriki wa shindano la kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti kati ya bia nyingine nne zinazotengenezwa na kampuni ya bia ya Serengeti ambapo mshindi aliibuka na kitita cha Tsh.100,000.  Shindano hilo ambalo lilifanyika Kihonda, mkoani Morogoro limemuibua mshindi wa jumla katika baa ya 18 Pub iliyopo mkoani humo. Kampeni ya Serengeti Masta imefikia mwisho kwa mkoa huo baada ya kudumu kwa muda wa miezi mitatu ikizunguka katika baa mbalimbali kutafuta wateja wanaoitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager. Sambamba na hilo kampeni hiyo ilijikita katika kutoa elimu kwa wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager.
Mshiriki wa shindano la mwisho la Serengeti Masta kwa wilaya ya Temeke ambaye alifanikiwa kuibuka mshindi wa kitita cha Tsh. 100,000/=Elisha Mwenga akionja ladha tofauti za bia za Serengeti ili kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la kumpata mshindi wa mwisho wa shindano hilo lililofanyika katika baa ya Kisuma ya Temeke jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii. (Kushoto) ni washiriki wenzake wakishuhudia zoezi zima.

Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Temeke Amani Kimaro (Katikati) akionyesha kiasi cha Tsh. 100,000/= ambayo alimkabidhi mshindi wa shindano la Serengeti Masta Elisha Mwenga (kulia) ambaye aliyewabwaga wenzake wane (4) katika kuitambua ladha halisi ya bia Serengeti Premium Lager wakati wa shindano hilo ambalo lilifanyika katika Baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii. (Kushoto) ni mshereheshaji wa shindano hilo Richard Godwin.
Mshiriki wa shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta kwa wilaya ya Temeke Emmanuel Nyaulingo (kulia) akipokea zawadi ya fulana kabla ya shindano hilo kuanza rasmi ambalo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam. (kushoto) ni balozi wa bia ya Serengeti Premium Lager Caroline Vincent na anayeshudia (katikati) ni mshereheshaji wa shindano hilo Richard Godwin. Kampeni hiyo inafikia tamati jijini Dar es salaam baada ya kumalizika mikoani pia ambapo imefanikiwa kuzifikia baa zaidi ya 200 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Kampeni.

Dar es Salaam, Kampeni ya “Serengeti Masta” iliyokua ikiendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti chini ya udhamini wa bia yake namba moja ya Serengeti Premium Lager, imefikia kilele jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki baada ya kampeni hiyo kuzunguka kwa muda wa miezi mitatu katika miji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Morogoro.
Katika kufunga Kampeni hiyo kwa kishindo, kwa kushirikiana mameneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, walijipanga kuwafikia mashabiki wengi zaidi wa bia hiyo ambapo iliwalazimu kufanya shindano la “Serengeti Masta” katika baa tatu zilizopo jijini Dar es salaam kwa siku tofauti.
Sherehe hizo ambazo zilionekana kuwafurahisha mashabiki wengi wa bia ya Serengeti Premium Lager, ziliambatana na burudani ya mziki, zawadi za fedha taslim, fulana na bia za bure.
Baadhi ya baa za jijini Dar es Salaam, ambazo zilizochaguliwa kuimalizia promosheni hiyo ni pamoja na Kisuma iliyopo Temeke, Zambezi Ubungo na Havana Park ya Segerea.
Akiizungumzia promosheni hiyo mmoja wa wateja maarufu wa bia ya Serengeti Premium Lager aliyehudhuria shindano la “Serengeti Masta” katika baa ya  Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam, Bw. Salehe Kitwana, aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti na mameneja wa bia hiyo, kwa kuibua kampeni ambayo imeweza kuwahamasisha wahudumu wa baa mbalimbali jijini Dar es Salaam na mikoani katika utoaji huduma bora kwa wateja wa bia hiyo, sambamba na kuwazawadia fedha taslim washiriki mbalimbali walioweza kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti baada ya bia hiyo kushindanishwa na bia nyingine tano zinazotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).
“Promosheni kama hii inawaunganisha mashabiki na kuwafanya waipende bia yao zaidi na zaidi pia nadhani huu ni mfano wa kuigwa na bia nyingine zinaweza kujifunza mengi kutokana na promosheni kama hii”.alisema Bw. Salehe
Naye Meneja Masoko wa bia ya Serengeti Premium Lager Bi. Anitha Msangi alisema,”Kampeni hii imekuwa ikiendeshwa kwa muda wa miezi mitatu sasa na kuanza kupamba moto baada ya mashabiki kuipokea kwa mikono miwili na kuifanya kuwa maarufu.
Alisisitiza kuwa, shindano la “Serengeti Masta” ni moja kati ya kampeni kubwa ambazo zimeweza kufanikiwa kiutekelezaji kwa mwaka huu, ikiwa ni moja ya kazi kubwa zilizofanywa na Kampuni ya bia ya Serengeti.
Bi. Msangi pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wateja wote wa bia ya Serengeti Premium Lager mameneja wa baa mbalimbali walioshiriki kwenye kampeni hii na wafanyakazi wote wa SBL nchi nzima kwa kuwaunga mkono na kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi zima la kampeni hiyo.
Aliongeza kuwa pamoja na ushiriki wa wateja kuwa mzuri lakini pia wamefanikiwa kuongeza mauzo ya bia ya Serengeti kufikia kiwango kikubwa kuliko hapo awali kwa mwaka huu.
Tafiti mbalimbali zilizofanywa na SBL katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hii imedhihirisha kuwa kampeni hiyo haikufaidisha tu kampuni ya bia ya Serengeti bali pia baa zaidi ya 4000 zilizotembelewa na shindano hilo nchi nzima katika kipindi chote cha miezi mitatu.
Vilevile kampeni hiyo imeibua washindi mbalimbali waliopewa cheo cha Serengeti Masta ambao walijizolea fedha taslim na bia za bure, fulana na zawadi mbalimbali.
“Namshukuru Mungu na sisi pia tumebahatika kuweza kuwa sehemu ya kampeni hii kabla ya kufikia tamati na ninajiona kama mwenye bahati sana” alisema Meneja wa baa ya Kisuma Thomas Kimaro ambaye alihojiwa na waandishi wa habari wakati wa shindano la mwisho la Serengeti Masta lililofanyika kwenye baa yake.
Kimaro aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwa mashuhuri wa kubuni mambo mapya kila kukicha na kuwasihi kuendelea kuleta promosheni kama hizi kwa kuwa zinaongeza mauzo ya bia hizo kwenye baa zao.                                                                                                              
Kampeni ya Serengeti Masta ilianzishwa mahususi kwa ajili ya kurudisha shukrani kwa wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager mara baada ya bia hiyo kushinda kinyang’anyiro cha bia ya kimataifa yenye viwango bora katika tuzo za “monde selection” za mwaka huu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.