Jokate Kumzalia AliKiba Mtoto Wa 4 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jokate Kumzalia AliKiba Mtoto Wa 4

Bet Sasa
Habari ‘hot’ iliyotua kwenye meza ya gazeti hili inadai kuwa, mwanamitindo ambaye ni Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ anatarajia kumzalia mpenzi wake wa sasa, Ali Kiba, Ijumaa lina kila kitu.
Ali-Kiba-na-Jokate
Hata hivyo, endapo atafanikiwa katika hilo, atakuwa amempa Kiba mtoto wa nne kwani tayari staa huyo wa Wimbo wa Mwana ana watoto watatu.
Kisikie chanzo
Akizungumza na Ijumaa kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, mmoja wa mashosti wa Jokate alisema kuwa, uhusiano wa mastaa hao umezidi kukua kadiri siku zinavyokwenda na mpango uliopo ni Jokate kubeba mimba ili kuwaziba midomo waliokuwa wakimsema vibaya.
“Unajua ile kapo ni nzuri na si unakumbuka Diamond aliwahi kumsema vibaya kuwa, hakutaka kumpa mtoto, mara hazai, sasa ameamua kumkomoa kwa kuzaa na Kiba na siku si nyingi mtasikia.
“Si Kiba ana watoto watatu ee, sasa Jokate atamzalia mtoto wa nne na mambo mengine yataendelea,” kilidai chanzo hicho.
Eti wanapika na kupakua
Chanzo kikaongeza kuwa, Jokate na Kiba mara nyingi wako pamoja na huwa mrembo huyo anakwenda kwa Kiba huko Kunduchi jijini Dar na kumpikia msosi.
“Ni kama walioamua kuziba masikio, wanapendana kweli na wameamua kuwa na maisha yao ila Jokate ni mtu wa siri sana, hapendi watu wajue mambo yao na hata hili la kubeba mimba itakuwa ni ‘sapraizi’,” kilidai chanzo.
Baada ya kupata umbeya huo, mwandishi wetu aliona ni busara kumpata Jokate ili kubalansi stori hii. Siku ya kwanza alipigiwa simu lakini hakupokea.
Siku ya pili alitumiwa sms ya kumsalimia na ndipo ‘chatting’ kati ya mwandishi na staa huyo ikawa hivi:
Ijumaa: Habari Jokate?
Jokate: Poa tu niambie una mpya gani maana nyie mnanilipua kila siku.
Ijumaa: Nimeona una bonanza umeliandaa kwa wanafunzi lina lengo gani?
Jokate: Yeah.. Bonanza hilo linafanyika kesho (Jumamosi) Viwanja vya Jangwani, lengo ni kuwakutanisha wanafunzi kwa ajili ya kuonesha vipaji vyao, itakuwa ni fursa ya kipekee.
Ijumaa: Sawasawa, nasikia siku hiyo ‘mr’ atakuwepo kutoa burudani.
Jokate: Nani?
Ijumaa: Si Ali Kiba, unazuga ee?
Jokate: Umeanza maswali yako ya kidaku, ndiyo maana sikupokeleagi simu zako.
Ijumaa: Tuachane na hilo, naomba unisaidie kitu kimoja, tumepata taarifa kuwa una mpango wa kumzalia Ali Kiba kwa sababu unampenda sana na lengo ni kumkomoa Diamond aliyewahi kukupaka kuwa ulimletea usanii kwenye suala la kumzalia. Hilo likoje?
Jokate: Hahaa!Umenichekesha kweli, mna mambo sana nyie, mimi sipendi kumuongelea kabisa Diamond yule ni zilipendwa, kuhusiana na swala la kuzaa mimi ni mwanamke na Kiba ni mwanaume kuzaa si jambo la ajabu na ipo siku nitaitwa mama.
Ijumaa: Sasa mbona kama unapinda? Weka wazi watu wajue, je unapenda kumzalia mtoto wa jinsia gani?
Jokate: Pliz naomba ukinitafuta, unitafutie mambo ya kazi.
Tujikumbushe
Huko nyuma Jokate aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond na walipoachana, wakarushiana maneno mazito ikiwa ni pamoja na Diamond kudai kuwa, Jokate alimletea usanii alipotaka amzalie.
Hata pale Jokate alipoamua kuhamia kwa Kiba, Diamond alirusha dongo kuwa, mshkaji wake huyo amechukua makombo na ndipo Kidoti alipomlipua na kumwambia kuwa, hana akili timamu.
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.