Je ni Busara Gani Alizotumia Bwana Mrema Kumnadi Mgombea Urais wa CCM Magufuli na si Mgombea urais Lyimo wa TLP. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Je ni Busara Gani Alizotumia Bwana Mrema Kumnadi Mgombea Urais wa CCM Magufuli na si Mgombea urais Lyimo wa TLP.

Ninataka niamini kuna muungano wa CCM na TLP kwani tukio la jana kati ya mgombea urais wa CCM na Mgombea Ubunge wa TLP ni tukio la aina yake. Kwangu nalipa nafasi ya kuitwa kituko cha jana.
1. TLP ina mgombea urais Bwana Lyimo. Sasa sijajua ni busara gani alizotumia Bwana Mrema Mgombea ubunge wa jimbo la Vunjo kumnadi Mgombea Urais wa CCM Magufuli na si Mgombea urais Lyimo wa TLP.
2. Ninatafakari ni busara gani alizotumia Mgombea Urais kumnadi Mgombea ubunge wa TLP jimbo la Vunjo wakati ana mgombea wake wa CCM.
3. Ninajiuliza kama ni muungano ni wa aina gani? Je! Lengo ni kuzigawa kura za UKAWA kupitia NCCR mageuzi kwa tiketi ya Mh. Mbatia?
4. Ninataka niamini kwenye siasa kuna vituko vingi kwanza vilianza vya matusi kupitia CCM vikaja vya kurukaruka, vikafuata mapushapu na sasa hili mwishoe mtasikia Mgombea amejiondoa kwenye kinyanganyiro dakika za mwisho heheheheeh.....
Vita yote hii ni ili tu UKAWA isipite kweli kazi CCM+TLP mnayo bora mjipange zaidi mmeonekana dhaifu na msio na mpango mzuri kwa kufanikiwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.