EMMANUEL MBASHA NI NANI ALIKUROGA ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

EMMANUEL MBASHA NI NANI ALIKUROGA ?

Ndoa na mapenzi ni mambo ambayo mara nyingi huwa hayaingiliwi,yametawaliwa na msemo kuwa'mapenzi ni wawili tu akiongezeka wa tatu ni mchawi',lakini pia huwa inapobidi watu wanaingilia hasa pale wahusika au mhusika mmoja anapovuka mstari mwekundu,
Hakuna asiyejua sakata la mbasha na mkewe flora,huyu jamaa alituhumiwa kumbaka shemeji yake,mmoja wa shahidi muhimu upande wa mashtaka alikuwa mkewe flora,ina maana flora alitaka mumewe aozee jela,na kweli wakati kesi ikiendelea flora alienda mahakamani na kutoa ushahidi wa kumkandamiza mumewe ili afungwe,
Mungu mkubwa hukumu ilipotoka mbasha kashinda kesi na sasa yupo huru,kilichoshangaza umma wa watanzania ni kauli ya mbasha kuwa bado anampenda sana mkewe flora na yupo tayari kuendelea kuishi nae,najiuliza kwa vitendo vyote alivyotendewa na huyo mwanamke bado anampendea nini?Huyu jamaa alirogwa?
Amerukwa na akili? Unampendaje mwanamke aliyetaka uozee jela? Watu wa karibu na mbasha msaidieni huyu jamaaa maana anakoelekea ni kutafuta kifo,msimcheke pls msaidieni tu.


Source: Jamii Forums...By The Counseller

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.