Dk Magufuli: TZ kama Ulaya Inawezekana - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dk Magufuli: TZ kama Ulaya Inawezekana

Bet Sasa

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema Tanzania inaweza kuwa kama nchi za Ulaya iwapo tu wananchi wataridhia aongoze Serikali ya Awamu ya Tano.
Dk Magufuli alisema hayo jana wakati akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa Mnadani, Sengerema mkoani hapa.
Dk Magufuli, ambaye alisema anagombea urais ili kuondoa umaskini kwa wote, aliahidi kutekeleza ahadi yake ya kufufua viwanda, hasa vya pamba, kuendeleza ujenzi wa barabara na kuongeza nafasi za ajira kwa vijana.
“Inawezekana Tanzania kuwa kama Ulaya,” alisema Dk Magufuli mbele ya maelfu ya watu waliofurika kwenye Uwanja wa Mnadani. “Nichagueni, nitahakikisha nafufua viwanda na vitajengwa vingine.
“Nataka pamba inayolimwa hapa iwe inauzwa hapahapa nchini, nguo tutatengeneza sisi wenyewe kwa kutumia viwanda vyetu.”
Pia alisema atajenga pia viwanda vingine kama vya kuchakata matunda ili kutengeneza juisi.
“Nawaambia ndugu zangu wa Sengerema, mimi ni mwenzenu nimefundisha shule ya sekondari ya hapa Sengerema. Sitawaangusha,” alisema mgombea huyo ambaye ni Waziri wa Ujenzi.
Alirejea kauli yake kuwa umasikini wa wengi unatokana na watu wachache kujilimbikizia mali kwa kujihusisha na rushwa na ufisadi.
Alisema maendeleo yaliyokuwepo zamani, hayafanani na ya leo, na kuwataka wananchi kuwabeza wanaosema serikali haijafanya kitu.
Alitoa mfano wa barabara zilizojengwa kuwa zimerahisisha usafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine, tofauti na ilivyokuwa zamani.
“Mimi Magufuli ndiyo nitakuwa rais?” aliwauliza wananchi ambao nao waliitikia, “ndiyo”.

-mwananchi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.