DK. MAGUFULI AMFAGILIA DIAMOND PLATINUMZ, IPO HAPA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

DK. MAGUFULI AMFAGILIA DIAMOND PLATINUMZ, IPO HAPA


RICHARD BUKOS, aliyekuwa Lindi
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amemmwagia sifa lukuki, mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi iliyopita nchini Marekani
Tukio hili lilitokea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili mkoani Lindi baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba kushuka jukwaani kukamua kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais, ndipo Magufuli alishika kipaza sauti na kumsifia Diamond aliyeshinda tuzo za Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Msanii Bora wa Mwaka na Utumbuizaji Bora wa Video.

“Ukweli nampongeza sana msanii Diamond kwa jinsi anavyojituma na kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu…,” alisema Magufuli huku pia akiwapongeza Ommy Dimpoz na Vanesa Mdee walioshinda tuzo tofauti katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha, katika kampeni hizo Magufuli aliwaahidi wakazi wa mji huo kuwajengea Lindi mpya ambayo itakuwa ya neema kupitia gesi inayopatikana kwenye ukanda huo, unafuu wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji ‘cement’ iliyoanza kupatikana kwa bei ya shilingi 8,000 kwenye kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara, zao la korosho ambalo Magufuli alijinandi kuwa na digrii ya zao hilo.


-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.