Diamond adai kolabo yake na Ne-Yo imewatisha wasanii wa Nigeria - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond adai kolabo yake na Ne-Yo imewatisha wasanii wa Nigeria

Diamond Platnumz amesema kolabo yake na msanii wa Marekani, Ne-Yo, imekuwa tishio kubwa kwa wasanii wa Nigeria.
diamond na Ne-Yo
Muimbaji huyo amesema Kcee na kundi la Bracket wameusikia wimbo huo na wakadata.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere akitokea Texas, Marekani katika utoaji wa tuzo za Afrimma, Diamond alisema muziki wa Tanzania unafanya vizuri hadi unawatia hofu wWanigeria.
“Wakati nipo Marekani juzi na Kcee, nikamsikilizisha nyimbo ambayo nimefanya na Ne-Yo, alikuwa na Bracket akachanganyikiwa sana! Akaniuliza ‘umemlipa shilingi ngapi?’, nikamwambia ‘mimi sijamlipa hata senti kumi’. Wenzetu wanafanya nyimbo zao na wasanii wakubwa lakini wao wanalipa. Sisi mwenyezi Mungu katupa bahati tunafanya nao nyimbo bureee,” alisema Diamond.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.