Breaking News:Diamond Awa Msanii wa Kwanza Afrika Kushinda ‘Worldwide Act Africa/India’ Kwenye Tuzo za MTV EMA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Breaking News:Diamond Awa Msanii wa Kwanza Afrika Kushinda ‘Worldwide Act Africa/India’ Kwenye Tuzo za MTV EMA

Diamond Platnumz ameiletea sifa na heshima kubwa Tanzania kwa mara nyingine, kwa kushinda tuzo kubwa ya ‘Best Worldwide Act Africa/India’ kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards 2015 zilizotolewa Milan, Italy usiku wa Jumapili Oct.25.


Hii ni kwa mara ya kwanza kwenye historia ya tuzo za MTV EMA toka vipegele vya Worldwide Act vilipoongezwa kwenye tuzo hizo mwaka 2011, tuzo ya ‘Best Worldwide Act Africa/India’ imekuja Afrika mwaka huu.

Diamond ambaye pia ni mshindi wa kipengele cha ‘Best African Act’ kwenye tuzo hizo, alikuwa akichuana na mwigizaji na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa pia Miss World mwaka 2000.

Ushindi wa Diamond ni mkubwa kwasababu hakuwa anaiwakilisha Tanzania pekee, bali bara zima la Afrika.

Hawa ni washindi wa miaka iliyopita wa kipengele alichoshinda Diamond mwaka huu:

2011 – Abdelfattah Grini (Morocco)
2012 – Ahmed Soultan (Morocco)
2013 – Ahmed Soultan (Morocco)
2014 – Mohammed Assaf (Palestina)

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.