Breaking News: Mgombea Ubunge ACT Arusha Mjini Afariki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Breaking News: Mgombea Ubunge ACT Arusha Mjini Afariki

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT) Estomih Malla amefariki dunia usiku wakuamkia leo katika hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro. 
Afisa habari wa ACT – Wazalendo, Abdallah Khamisi ameiambia MwanaHalisi Online kuwa taarifa za kutokea kifo hicho walizipata usiku majira ya saa kumi kuwa kati ya saa saba hadi saa nane usiku mgombea huyo alipatwa na umauti.
Taarifa ya awali iliyotolewa na Afisa habari huyo zimesema kuwa Malla alianza kuumwa kichwa ghafla Oktoba 6 mwaka huu siku ambayo Mgombea wa Urais kupitia chama hicho Anna Mghwira alikuwa ziarani Arusha kujinadi na kuwanadi wagombea wengine wa Udiwani na Ubunge.
“Alipatwa na homa ya kuumwa kichwa ghafla, akashindwa kupanda jukwaani kisha akakimbizwa hospitalini, hii ilikuwa ni muda mchache kabla Mgombea wetu wa Urais kuanza kumnadi kwenye mkutano wake uliofanyika Arusha” amesema Khamisi.
Khamisi ameiambia MwanaHalisi kwa ACT-Wazalendo watakutana leo Jijini Dar es Salam ili taratibu za mazishi na masuala mengine yaweze kujulikana baada ya kikao hicho.
-MwanaHalisi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.