BREAKING NEWS: MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI KWA AJALI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

BREAKING NEWS: MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI KWA AJALI

Mchungaji Mtikila Enzi za uhai wake 

Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia kwa ajali ya Gari leo Majira ya saa 10 alfajiri akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni .

 Taarifa zilizothibitishwa na mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini na mwenyekiti wa DP Mkoa Robart Kisinini zimesema ni kweli mwenyekiti wake huyo Taifa amefariki dunia 

, RPC Pwani amesema ni kweli kuna ajali imetokea eneo la Msolwa ameenda kwenye eneo la tukio na atatoa taarifa baadae

Ajali hiyo imetokea  eneo la Msolwa mkoani Pwani huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa taarifa zaidi ataitoa baada ya kurejea kutoka  eneo la tukio .

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.