Birthday Ya Diamond Pombe, Mademu, Bata La Nguvu Balaa, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Birthday Ya Diamond Pombe, Mademu, Bata La Nguvu Balaa, Ipo Hapa

Usipime! Ndugu, jamaa na marafiki wa staa bab’kubwa Afrika Mashariki na Kati, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, wikiendi iliyopita wamekula bata la hatari katika sherehe ya kuzaliwa kwa msanii huyo, Ijumaa Wikienda linaripoti.
Burudani na raha hizo zilifanyika nyumbani kwa Diamond, Madale- Tegeta jijini Dar, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita na kuhudhuriwa na mastaa kibao.
‘Diamond Platnumz’, akimwagiwa Soda na meneja wake.
MADEMU, VINYWAJI VYATAWALA
Huku likiwa na mwaliko rasmi, gazeti hili liliwashuhudia mademu ‘classic’ wakijiachia mjengoni humo huku vinywaji laini na pombe kali vikichukua nafasi kubwa katika suala la burudani.
Mbali na hayo, baadhi ya waliofika kwenye hafla hiyo walijivinjari kwa kuogelea, kucheza muziki, kupiga mitungi na kadhalika hivyo kufanya shughuli hiyo kugubikwa na shangwe ya kufa mtu.
MAZINGIRA RAFIKI
Mazingira ya nyumbani kwa Diamond yaliwafanya karibu wageni wote waliofika kwa mara ya kwanza kujisikia burudani, kwani Diamond alionekana kujipanga na kupafanya nyumbani kwake kuwa ni mji wenye heshima ya kistaa tofauti na nyumba nyingi za mastaa wengine wa Bongo.
…Akikata Keki
FULL VINYWAJI
Eneo la kaunta iliyopo pembeni mwa bwawa la kuongelea lilikuwa limefurika kwa vinywaji kiasi kwamba hakuna mgeni aliyehitaji kinywaji na kukosa.
MASTAA WALIOIBUKA
Baadhi ya mastaa waliojitokeza katika sherehe hiyo ni pamoja na Salama Jabir, Rita Paulsen ‘Madam’ Ambwene Yessayah ‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Hamis Mandi ‘B-Dozen’, Shadee Weris, Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’, Babu Tale, Fella na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alitinga mahali hapo usiku mnene na kujumuika na mastaa hao kwa burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea.
Shilole nae alikuwepo.
BETHIDEI YENYE WADHAMINI
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa mameneja wa Diamond, Salam alisema kwamba, maandalizi ya sherehe hiyo yalifanikishwa na uongozi wake huku wakipigwa tafu kubwa na wadhamini wao ambao ni Kampuni ya Cocacola na Serengeti.
Alisema kuwa makampuni hayo yaliwapatia vinywaji mbalimbali huku Diamond akitia mkono wake kufanikisha sherehe hiyo na kufanya gharama zote za kuandaa shughuli hiyo kuwa zaidi ya Sh. milioni 10.
“Kwenye maisha naamini huwa hakuna sherehe ndogo, hatukuwa na mpango wa kufanya sherehe kabisa lakini tumejikuta tukifanya haya yaliyojiri, wazo hili lilitujia ghafla, tukaamua kuwahusisha wadau wetu na kutupatia baadhi ya vinywaji na sisi kama uongozi wa Diamond tukaamua kuingiza mkono wetu.
“Nafurahi sana kuona watu ‘wame-enjoy’ vya kutosha. Kiukweli hakuna aliyetarajia kama ingekuwa kubwa kiasi hiki,” alisema Salam na kuongeza: “Namshukuru Mungu tumemaliza shughuli kwa amani na hadi alfajiri hii naona watu wanaondoka, hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa wala kuibiwa, najua mapungufu huwa hayakosi kwa kila kitu ila nitumie fursa hii kuwashukuru wote waliojitokeza na kufanikisha kwani gharama za shughuli hii ukijumuisha na wadhamini zinaweza kuwa zaidi ya milioni kumi.”
DIAMOND ANENA
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye pati hiyo.
“Namshukuru Mungu kwa kuendelea kunilinda hadi kufikia tena siku hii muhimu maishani mwangu, sina la zaidi ila nawashukuru tu wote waliojitokeza kusherekea na mimi.
“Kuna walioacha usingizi na familia zao, wengine wametoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na kujumuika nami, hiyo ni ishara ya mapenzi ya dhati na upendo, nawashukuru wote waliofanikisha sherehe hii, bila wao nisingeweza kufanya kila jambo,” alisema Diamond.Makabrasha ya gazeti hili yanaonesha kuwa, Diamond sasa ametimiza umri wa miaka 26 tangu alipoliona jua Septemba 2, 1989.

PICHA ZAIDI > BOFYA HAPA <

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.