Beckham na Zidane kurejea uwanjani November kwenye mechi ya Hisani ya Mastaa Wote - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Beckham na Zidane kurejea uwanjani November kwenye mechi ya Hisani ya Mastaa Wote

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, David Beckham atakuwa nohodha wa timu ya Uingereza na Ireland itakayokuwa na mastaa wote kucheza na timu ya dunia na inayoongozwa na Zinedine Zidane kwenye mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford, Jumamosi, November 14 ili kukuza uelewa na fedha kwaajili ya shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF.
Generated by  IJG JPEG Library
Zidane na Beckham walipokuwa Real Madrid
Timu hizo zitanolewa na makocha wawili wenye heshima kubwa kwenye soka duniani, Sir Alex Ferguson na Carlo Ancelotti.
Beckham na Zinedine wataungana na wachezaji wengine nyota wa zamani kwenye mtanange huo uliopewa jina ‘Match for Children.’
Refa nguli wa Italia Pierluigi Collina, aliyewahi kushinda mara sita tuzo ya FIFA ya ‘Best Referee of the Year’ atacheza mchezo huo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.