Barnaba Ampa Bonge La Ushauri Mrembo Lulu ..Soma Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Barnaba Ampa Bonge La Ushauri Mrembo Lulu ..Soma Hapa

Barnaba Elias ameusifia uigizaji wa Elizabeth Michael aka Lulu lakini amemtaka kubadilika na kutafuta aina moja ya uigizaji ambao utakuwa unamtambulisha.
Lulu michael
Akizungumza na kipindi cha DJ Show cha Radio One, Barnaba alisema anapenda kuangalia filamu za kibongo na anashangaa kuona watu wanabeza kazi hizo.
“Lulu anafanya vizuri lakini atambue anatakiwa kutafuta sehemu moja anayofiti, jinsi anavyokuwa mkubwa yanahitajika mabadiliko,” alisema.
“Mimi nashangaa watu wanaosema filamu za Bongo sio nzuri, mimi ni mpenzi mkubwa wa filamu za Bongo na sipendi kupitwa na movie yoyote. Hata nikisafiri kokote lazima niwe na filamu za kutosha za kuangalia, napenda sana za vichekesho na nyingine.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.