Baada ya Kutoka Hijja: Majuto Hafanyi Tena Filamu za Aina Hii - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Kutoka Hijja: Majuto Hafanyi Tena Filamu za Aina Hii

Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini, Alhaj Athumani King Majuto, amesema baada ya kwenda kuhiji Mecca, atakuwa hafanyi tena filamu ambazo ndani yake kutakuwa na matendo ya kumchukiza Mungu.
“Sasa hivi filamu kama za kunywa pombe au kuna matukio ya kumchukiza Mungu siwezi kufanya,” Majuto ameiambia Bongo5.
“Lakini ambazo zitakuwa hazima matukio kama hayo nitaendelea kufanya. Mimi sasa hivi ni Alhaj, natakiwa kuwa mfano kwa kumcha Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha watu kufanya mambo mema,” ameongeza.
Chanzo: Bongo 5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.