AliKiba na Hasheem Wagongana Kumuoa Jokate, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

AliKiba na Hasheem Wagongana Kumuoa Jokate, Ipo Hapa

Mastaa katika category tofauti, Ali Saleh Kiba na Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA), Hasheem Thabit Manka, wanadaiwa kuchuana vikali kila mmoja akiwania kumuoa mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ huku mama mzazi wa mrembo huyo akitia ngumu, Risasi Jumamosi linaweza kuripoti.
TAARIFA ZA AWALI
Habari za awali, zilizovujishwa na mtoa taarifa wetu ambaye ni rafiki wa karibu na familia ya Jokate, juzi Jumatano zilieleza kwamba, kwa sasa kuna vita baridi kati ya Hasheem na Kiba kwa kila mmoja kutumia njia mbadala ili kuhakikisha anamuweka kibindoni mrembo huyo.
MPASUKO NDANI YA FAMILIA
“Lakini wakati hilo likiendelea, kuna taarifa kwamba kuna mpasuko kwenye familia ya Jojo (Kidoti). Inasemekana mama wa mrembo huyo anampa nafasi kubwa Hasheem.
“Lakini kwa upande wake, Jokate amekuwa akimnadi Kiba, jambo linalozua mpasuko mkubwa kwa familia hiyo,” kilinyetisha chanzo hicho.
Chanzo hicho kilishusha madai mazito kwamba, hivi karibuni baada ya Hasheem kusikia tetesi za kushamiri kwa penzi la Kiba na Jokate, alidaiwa kukwea pipa kutoka Marekani kisha akatua Bongo kimyakimya ambapo alifika nyumbani kwa akina Jokate, Oysterbay jijini Dar ili kujua mbivu na mbichi.
“Baada ya kuona hivyo, mama Kidoti aliitisha kikao cha dharura na kumtaka Jokate akubali kuolewa na Hasheem ili waishi maisha mazuri lakini bidada (Jokate) alilipinga vibaya na kushikilia alichokiita uhuru wa mapenzi na kwamba chaguo lake ni Kiba.
“Kiukweli hali mbaya sana kati ya Jokate na bimkubwa wake, mama anataka binti aolewe na Hasheem lakini Jokate anashikilia msimamo wa kuwa na Kiba,” kilinyetisha ‘kikulacho’ hicho.
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.