Afande Sele Kuweka Muziki Pembeni, Kugeukia Kilimo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Afande Sele Kuweka Muziki Pembeni, Kugeukia Kilimo

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amesema ameamua kuweka muziki pembeni ili kujikita kwenye kilimo na ufugaji.
Afande-Sele-nzuri_full
Rapper huyo wa ‘Darubini Kali’, aliyeshindwa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo la Morogoro mjini kupitia chama cha ACT, ameiambia Bongo5 kuwa anaamini hawezi kufanya muziki wa kibiashara utakaomlipa kutokana na kuwagawa mashabiki wake kupitia siasa.
“Kusema kweli kwenye mambo ya muziki niwe mkweli kwamba sijajiandaa vyovyote,” amesema Afande.
“Kwa sababu akili yangu ilikuwa imeshakimbilia kwenye siasa, kwahiyo kuhusu suala la muziki ni kama vile niweke pembeni na nijikite zaidi kwenye masuala ya kilimo cha mboga mboga, matunda pamoja na ufugaji,” ameongeza.
“Kwenye muziki kuna mambo mengi sasa hivi, watu wanataka muziki wa kukimbia na kwa hali ya sisi ambao tulijikita kwenye siasa tumeshatengeza makundi, sasa yale makundi kuyafanya yawe kitu kimoja na kuweza kusupport muziki wa kwetu ambao unaundwa na mashairi ya kiharakati, sitegemei kama unaweza kuwa muziki wa kikazi kama zamani. Sasa hivi ukisikia nimetoa muziki nimepata mashairi ndio nitafanya kwa sababu muziki ni maisha na upo kwenye damu.”

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.