50 Cent Aringishia Mabunda ya Dola 100 Instagram Kuthibitisha kuwa Hajafilisika ! Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

50 Cent Aringishia Mabunda ya Dola 100 Instagram Kuthibitisha kuwa Hajafilisika ! Ipo Hapa

Baada ya 50 Cent kutangaza kuwa amefilisika mwezi July mwaka huu, ameibuka na kuringishia mabunda ya dola mia mia kwa followers wake zaidi ya milioni 6.5 wa Instagram.
Siku chache baada ya kuripotiwa kuwa jumba lake la kifahari ambalo alitangaza kuliuza kwa dola milioni 18.5 mwaka 2007 kushushwa bei na sasa linauzwa kwa dola milioni 8.5, 50 ameamua kuwadhihirishia watu kuwa akaunti zake za benki bado zimenona.
50 2
50 Cent alishare video akiwa amejifunika miguu yote na mabunda ya dola na kuandika, “Cold in my eyes, ashy knuckles…I hustle so hard, I can’t see me legs. LMAO SOUTHSIDE ALL DAY LETS GET IT!!! #EFFENVODKA #FRIGO #SMSAUDIO,”
Muda mfupi baadae alipost picha akiwa ametandaza mabunda ya dola kitandani kwake na kuandika “Ok I found my legs, but I can’t find nothing to watch on TV. Power season 3 on the way. #EFFENVODKA #FRIGO #SMSAUDIO.”
50 3
Hakuishia hapo, 50 alipost picha nyingine akiwa amezipanga dola kwa kuandika neon ‘BROKE’ kama ishara ya kuwaambia watu hajafilisika, huku akiweka caption kuwa hizo ni za lunch tu.
“’Man this lunch money, I gotta go to work I’m still up, no Sleep at all. NEW MUSIC this week,Off The KANAN tape. #EFFENVODKA #FRIGO #SMSAUDIO.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.