WEMA SEPETU AMUANIKA MWANAUME ATAKAYEZAA NAYE, AMWAGIA SIFA KIBAO - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

WEMA SEPETU AMUANIKA MWANAUME ATAKAYEZAA NAYE, AMWAGIA SIFA KIBAO


BAADA ya kupita ukimya mrefu bila kuzungumzia mapenzi, mrembo asiyepoteza ubora wake, Wema Sepetu ‘Madam’ amemtaja mwanaume anayetarajia kumzalia mtoto kuwa ni Luis Munana, raia wa Namibia. Wema alifunguka hayo juzikati mara baada ya mwandishi wetu kutaka kujua ana mpango gani kwenye ulimwengu wa ‘malovee’ ndipo alipomwanika Luis kuwa ndiye mwanaume pekee ambaye ameshafikia hatua ya kumuamini na yuko tayari kuzaa naye kwa namna yoyote licha ya kujua ana tatizo la uzazi.
“Luis ndiyo kila kitu kwangu, ndiye mwanaume ambaye tunaelewana na siyo mswahili kama kina mwafulani. Luis nitazaa naye hata kwa ku-adopt (kuasili) mtoto kama njia za kawaida zitashindikana, ndiye mwanaume ambaye nimepanga aje kuwa baba wa watoto wangu,” alisema Wema.
Kabla ya kufunguka hayo, Wema alikuwa akimposti mwanaume huyo ambaye alishiriki Shindano la Big Brother-Hotshorts (2014) kwenye ukurasa wake wa Instagram pasipo kuandika kama ni mpenzi wake lakini kwa sasa ameamua kuweka kila kitu hadharani.
Miezi kadhaa iliyopita, Wema aliwahi kuonekana na Luis katika pati ya Instagram iliyofanyika kwenye Viwanja vya Posta jijini Dar kisha wawili hao kudaiwa kulala pamoja katika hoteli moja jijini humo.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.