SIASA: Mastaa na Uchaguzi 2015 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

SIASA: Mastaa na Uchaguzi 2015

Bet Sasa
Kampeni zinaendelea vizuri katika kila upande na hata yale maneno yanayoongelewa ni utani kama ule uliop kwenye timu za mpira wa Yanga na Simba, changamoto kubwa iliyopo ni kwa wapiga kura kwa sababu wanatakiwa kuangalia sera muhimu kama afya na elimu kutoka kwa wagombea wao.
Kwangu naona muelekeo wa kampeni ni mzuri lakini tunaomba hali ya amani na utulivu iwe hivi hivi mpaka siku ya uchaguzi itakapofika ili tupate kuchagua viongozi sahihi watakaotuwakilishia matatizo yetu huko bungeni.
Muonekano wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu uko vizuri sana tu sema wanatuharibia wale watu wanaotumia muda huu kutoa kauli chafu zenye kuwakera watu badala ya kutangaza sera muhimu kwa wananchi kwa sababu wao ndiyo waamuzi.
Kampeni za mwaka huu ni tofauti na za miaka iliyopita kwa sababu  kuna muamko mkubwa kutoka kwa akina mama na vijana ambao wengi wao wana kiu ya kupata mabadiliko na hata idadi ya wapiga kura nayo inaonekana kuwa kubwa.
Makala by Shani Ramadhani :GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.