Rwanda Miongoni Mwa Nchi Salama Zaidi Duniani, soma hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rwanda Miongoni Mwa Nchi Salama Zaidi Duniani, soma hapa

Kigali, mji mkuu wa Rwanda
Kigali, mji mkuu wa Rwanda
Rwanda imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye amani na usalama zaidi duniani kwa raia wake.
Hayo yamo katika ripoti ya Shirika la uchunguzi wa maoni la Gallup ya mwaka huu ambapo Rwanda imewekwa katika orodha ya nchi ambazo zina usalama zaidi duniani.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa, barabara za Rwanda zina anga ya usalama kwa ajili ya wapita njia hata katika nyakati za usiku.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali, Rwanda
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali, Rwanda
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi ya Singapore inashikilia nafasi ya kwanza duniani kwa nchi zenye amani na usalama kwa raia wake.
Kutajwa Rwanda katika orodha ya nchi zenye amani zaidi kwa raia wake, kunaifanya nchi hiyo izidi kung’ara kimataifa hasa baada ya miaka ya hivi karibuni kusifika katika kupambana na ufisadi na kupiga hatua kubwa katika uga wa ustawi na maendeleo.
-Redio Iran

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.