REGINALD MENGI AJITOA RASMI KWA LOWASSA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

REGINALD MENGI AJITOA RASMI KWA LOWASSA

Bet Sasa
Tangu mbio za Urais zianze kushika kasi mkurugenzi wa IPP Media ndugu Regnald Mengi alionekana wazi wazi kuiunga mkono timu ya UKAWA
Ghafla Mkurugenzi huyo ameamua kujitoa kwenye timu hiyo baada ya kuona anapoteza nguvu zake wakati ana uhakika wa 100% kuwa Magufuli ndiye Rais wa awamu ya tano. Mengi amesema haoni faida ya kupoteza muda wake kumuunga mkono mtu mwenye uhakika wa kushindwa. Mengi amekubali wazi kuwa ushindi wa kiti cha Urais 2015 ni wa Magufuli... "kama hawa jamaa watashinda nafasi ya Urais basi ni baada ya miaka 10 siyo hivi sasa, huu mwaka ushindi utakuwa wa Magufuli tu tutake tusitake"
Pigo kubwa kama hilo limeambatana na kuondoka kwa wasanii mbalimbali waliotimkia kambi ya Ndugu Magufuli akiwemo Aunt Ezekiel, Ray na Juma Nature. Mshirika wake mkuu Hussein Bashe nae amejiweka pembeni na kuutangazia umma kuwa "ili wananchi wawe salama ni lazima kiti cha urais kikabidhiwe kwenye mikono salama, kinyume chake wananchi hawatokuwa salama, na mikono salama ni ya ndugu Magufuli tu"

Mwaka wa kufa nyani miti yote huteleza, EDO keshaanza kufa na miti yake pia imeanza kuteleza taratibu

By Aisha Idd/Jamii Forums

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.