RAY C "KUNA WATU WANATAKA KUNIUA, NI MTIHANI TU KWA BINADAMU" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

RAY C "KUNA WATU WANATAKA KUNIUA, NI MTIHANI TU KWA BINADAMU"

Yamekuwa hayo tena! Staa wa muziki Bongo, Rehema Chalamila `Ray C’ yupo kwenye hofu nzito ya kutaka kuuawa kwa kile alichodai ni chuki za binadamu wasiomtakia mema.
Wikiendi iliyopita Ray C alitupia ujumbe mzito mtandaoni uliosomeka: “Nacheka lakini sina furaha ila najua kabisa mpango wao kwangu ni kuniua kabisa nipotee! Sitakufa bali nitaishi! Nashukuru kuwa ninajua haki yangu!
“Ndiyo chanzo chote cha chuki na fitina! Ila kumbukeni na ninyi mna watoto pia muombeni Mungu awaepushie hili balaa ndani ya familia zenu ila kumbukeni tu kuwa malipo ni hapahapa duniani tena siku wala si nyingi.”
Ilielezwa kwamba, Ray C alitoa ujumbe huyo akiwalalamikia watu ambao wamekuwa wakimnyima dozi ya Methadone ya kuondoa sumu ya madawa ya kulevya mwilini.Akichati na gazeti hili, Ray C alisema hiyo yote ni mtihani tu kwa binadamu.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.