PICHA: Usher Raymond kafunga ndoa kisiri siri, wapo nchini Cuba kwa honeymoon . - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

PICHA: Usher Raymond kafunga ndoa kisiri siri, wapo nchini Cuba kwa honeymoon .

grace-usher
Usher Raymond Na Mke Wake Grace Miguel
Mtandao wa US Weekly umeripoti kuwa R&B super staa kutoka Marekani Usher Raymond  amefunga ndoa kisiri siri na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye wamekuwa pamoja toka mwaka 2009.
Dada huyu ambaye anafahamika kama Grace Miguel ni meneja wa Usher na kazi zake.
Taarifa nilizopata ni kwamba Usher amekuwa akificha siri toka mwanzoni mwa mwezi september walipofunga ndoa na mpenzi wake wa miaka mitano Grace Miguel na wameonekana nchini Cuba kwenye fungate yao ‘Honeymoon’.
Fahamu kuwa Usher ana watoto wawili kutoka kwenye ndoa yake ya mwanzo na mwana mamaTameka Foster na watoto wake ni Naviyd Ely mwenye miaka 6 na Usher Raymond V mwenye miaka 7.
usher 3
Picha kutoka kwenye Instagram ya Grace Miguel akiwa na Usher Raymond kwenye honeymoon yao Nchini Cuba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.