Nay wa Mitego Amvaa January Makamba..Adai January Ndio Mnunuzi Mkuu wa Akina Dr Slaa, Lupumba, Twaweza na Wasanii - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Amvaa January Makamba..Adai January Ndio Mnunuzi Mkuu wa Akina Dr Slaa, Lupumba, Twaweza na Wasanii

Msanii  wa  bongo  fleva, Nay  wa  Mitego  amemvaa  mjumbe  wa  kamati  ya  Kampeni  ya  CCM,January  Makamba  na  kudai  yeye  ni  mnunuaji  mkuu  wa  tafiti  na  wasanii  kwa  lengo  la kukisaidia  chama  chake.

Nay  alimjibu  January  Makamba  aliyepost  ujumbe  ukionyesha  kushangaa  tuhuma  dhidi  ya  CCM  kuwa  imekuwa  ikinunua  wanasiasa,tafiti  pamoja  na  wasanii  kwa  lengo  la  kuulaghai  umma.

"Zitto kanunuliwa. Slaa kanunuliwa. Lipumba kanunuliwa. Twaweza imenunuliwa. Synovate imenunuliwa. Wasanii wamenunuliwa. Tuwe creative kidogo" Aliandika  January  Makamba.

"Ni kabisaa kwani uongo? We ndo mnunuzi mkuu. Bro kama ubunifu ni hela basi we Master wa Ubunifu... @JMakamba Ongeza ubunifu bro" Alijibu  Nay  wa  Mitego.


-udakuspecially

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.