Mtoto Wa Paul Walker Aishtaki Kampuni Ya Porsche, Sababu zipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mtoto Wa Paul Walker Aishtaki Kampuni Ya Porsche, Sababu zipo Hapa

Bet Sasa
Mtoto wa kike wa Paul Walker anaishtaki kampuni ya Porsche, kwa kudai kuwa gari hilo la michezo lililomuua baba yake miaka miwili iliyopita lilikuwa na kasoro za utengenezaji.
Paul-Walker-in-Car-Race
Mashtaka hayo yaliyowasilishwa Jumatatu hii na Meadow Rain Walker yanataka kulipwa kwa hasara ambazo hazijatajwa kwa makosa ambayo wanasheria wake wanadai yalimfanya muigizaji huyo kunaswa kwenye gari hiyo aina ya Porsche Carrera GT baada ya kuanguka na kuwaka moto November 2013.
Mashtaka hayo yanadai kuwa gari hilo lililokuwa likiuzwa kama la mashindano ya mtaani, halikuwa na mfumo imara wa control na kumlinda abiria na kuzuia kushika moto pale linapoanguka.
Kifo cha Walker kilitokea wakati wakiwa wamepumzika kwa muda kushoot filamu ya “Fast & Furious 7.”

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.