MPYA: Nicki Minaj ‘Kuipa Dunia Kile Inachotaka’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MPYA: Nicki Minaj ‘Kuipa Dunia Kile Inachotaka’

Bet Sasa
Nicki Minaj ameahidi kuipa dunia kile inachotaka
Nicki Minaj ameahidi kuipa dunia kile inachotaka
Nicki Minaj anatanua vipaji vyake vya muziki kwenda kwenye televisheni.
Muimbaji huyo wa Anaconda, 32, anajiandaa kuwa staa na mtayarishaji mkubwa wa mlolongo wa kipindi cha kuchekesha kwenye runinga ya ABC.
Tangazo alilotuma kwenye ukurasa wake wa Instagram
Tangazo alilotuma kwenye ukurasa wake wa Instagram
Maisha ya Nicki yanatoa hamasa kwani kipindi hiko kitamuonyesha alivyoibukia kwenye ustaa wa muziki ikiwemo kuhama kwa familia yake kutoka Trinidad mapema mwa miaka ya 1990 wakati alipokuwa mdogo na kukulia Queens, New York.
Staa huyo ambaye ni maarufu kwa kuvaa nguo zinazoonyesha na hasa akiwa jukwaani, ameahidi ‘kuipa dunia kile inachotaka,” Entertainment Weekly iliripoti.
Minaj ataigiza kuhusu maisha yake ya muziki kwenye televisheni ya ABC
Minaj ataigiza kuhusu maisha yake ya muziki kwenye televisheni ya ABC
Siku ya Jumanne, alitangaza tangazo hilo la ABC kwenye ukurasa wake wa Instagram, lililosomeka: : ‘BREAKING NEWS! @Nicki Minaj is executive producing & appearing in a new @ABCFamily comedy based on her life!’

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.