Mnyika Awaumbua Watanzania Na Kumtwanga Rafiki Yake Dr. Slaa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mnyika Awaumbua Watanzania Na Kumtwanga Rafiki Yake Dr. Slaa


Mgombe ubunge kwa kupitia UKAWA kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika, jana ameonyesha kuwa hata yeye haungani mkono na rafiki wake wa karibu Dr Slaa, na kumwita Samson aliye shawishiwa na Delila kukisaliti chama.
"Si mnamkumbuka Samsoni wetu aliyedanganywa na Delila..? anayesema sisi tumehamisha uchafu chooni na kuuweka sebureni..? sasa sisi na yeye nani atakuwa sehemu safi kati ya yeye aliyetoka sebureni na kuenda kukaa chooni na sisi tukachukua uchafu kidogo wa chooni.? yeye ndio yuko sehemu chafu zaidi kwani sisi tunamchukua mchafu tunamsafisha na kumkaribisha sbuleni na mwisho chumbani kabisa" alisema Mnyika
Aliyasema haya akiongea kwenye mkutano uliofanyika jana viwanja vya Mbezi mwisho jimbo la Kibamba ambako mgombea urais Lowassa alikuwa ananadi sera zake kwa wananchi wa jimbo hilo.
Hata hiyo aliendelea kuwataka watanzania kumpuuza kwani ni kati ya watu wanaotumika na CCM ili kujinasua na mtikisiko inaoupata na ndio maana inawashambulia saana waliohama kutoka CCM na kujiunga na upinzani.
Hii ilikuwa ni fimbo kubwa saana kwa watanzania wanaovumisha kila siku kuwa Mnyika anamuunga mkono Slaa na mitandao ya kijamii kuandika saana kuwa hata yeye yuko mbioni kukihama chama cha CHADEMA.
Hata hivyo alimwahidi mgombea urais wake ushindi katika kata zote, ubunge na kupata kura nyingi za urais kutoka katika jimbo lake.

Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.