Mke Acharuka na Kusema ..Jack Wolper Niachie Mume Wangu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mke Acharuka na Kusema ..Jack Wolper Niachie Mume Wangu

Chanzo makini kimelieleza Ijumaa Wikienda kwamba, baada ya habari na picha za Wolper na Mkongomani huyo kuripotiwa na gazeti ndugu na hili, Risasi Jumamosi, mke wa ndoa wa mwanaume huyo alijitokeza na kuvunja ukimya akimtaka mwigizaji huyo aachane na mumewe huyo mara moja kabla hajamchukulia hatua za kisheria kwa sababu ameingilia ndoa yake.

“Unajua baada ya ninyi (Global) kuanika picha za Wolper kwenye gazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii akivishwa pete ya uchumba na Mkongomani, mke wake ameshindwa kuvumilia hivyo amelazimika kumtumia ujumbe Wolper akimtaka aachane na mume wake  kwani kama alikuwa hana taarifa kuanzia leo (Jumamosi) atambue kwamba huyo mwanaume ni mume halali wa mtu na ana watoto ndani ya ndoa.

“Yaani mke wa Mkongomani amemjia juu Wolper akimtaka amwachie mumewe, ajiweke pembeni mara moja na kama alidanganywa kuwa huyo mwanaume hajaoa, basi atambue kwamba tayari alishafunga naye pingu za maisha, tena kanisani na tayari ana familia ya watoto wawili, haoni sababu ya kumnyamazia maana ameumia sana hivyo anamtahadharisha ili baadaye asije akaanza kulia akisema hajaambiwa,” kilisema chanzo hicho.

MSIKIE WOLPER

Ili kuweka mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wolper ili kujua kama ameshayapata malalamiko hayo ambapo alifunguka kuwa, kuna maneno mengi yanazungumzwa juu ya tukio hilo lakini ukweli wa mambo zaidi anaufahamu yeye na mchumba’ke huyo hivyo haoni sababu ya kumwambia kila mtu maana mpaka anafikia uamuzi wa kuvishwa pete tayari walishajadiliana vya kutosha.

“Naweza kusema kwamba ni moja ya historia katika maisha ya mchumba wangu hivyo hata nilipoona hizo picha za mkewe hakuna jambo lililonishtusha kwani tayari alikuwa ameshaniambia juu ya misukosuko aliyoipitia kwenye ndoa yake huko nyuma.

“Hadi anafikia hatua ya kunivisha pete basi watu wanatakiwa kujua tu kwamba kila jambo liko sawa na zaidi wao wanatakiwa kusubiri hadi siku ya ndoa yetu waone kama itafungwa au lah.

“Siku hizi dunia imekuwa kama kijiji hivyo huwezi kuwazuia watu kuongea jambo, mchumba wangu ananijua na mimi ninamjua kwa kina, pamoja na kwamba watu pia wamekuwa wakimletea maneno kuhusu mimi lakini nimemwambia aachane nao kwani hakuna sababu ya kujibizana nao, kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kutumia kinywa chake jinsi anavyoweza maana ningekuwa sijui background (maisha ya nyuma) yake kweli baada ya kuona hizo picha za mkewe na maneno ya watu wanayosema ingeniuma sana.

“Nafikiri watu wanachotakiwa kujua juu yetu ni kwamba Mungu akishapanga jambo kamwe binadamu hawezi kulipangua hata iweje na kwa maana hiyo sasa hata mwanaume akishakupenda ni ngumu kumsikiliza mtu mwingine maana upendo wa mtu ni moyo na nafsi yake mwenyewe ndiyo inayoweza kumuongoza kwa kila hali.

“Watu wameshafanya kila juhudi za kutugombanisha lakini sasa ameshazoea hadi anavichukulia kama burudani tu, hata mimi haya ninayaona kama matangazo ya biashara hivyo hakuna linaloniumiza kichwa,” alisema Wolper.

ETI ANA GUNDU?

Kutokana na kitendo hicho wadau mbalimbali walifika mbali na kudai kwamba mwanadada huyo inawezekana ana gundu kwani ameshakuwa na wanaume tofauti na wengine kumvisha pete ya uchumnba na kutambulishana kwa wazazi lakini ikawa ndivyo sivyo.

“Wolper anatakiwa kujiangalia sana na kumuomba Mungu kwani siyo mara ya kwanza kuwa na wanaume wa watu, kinachowaponza hawa mastaa wetu wana tamaa sana ya fedha ambazo huwasababisha kuwa na mtu kwenye uhusiano bila kumchunguza vizuri,” alisema mdau mmoja mkazi wa Mwenge, Dar.

TUJIKUMBUSHE

Kwa Wolper, kuvishwa pete ya uchumba siyo mara ya kwanza kwani awali aliwahi kuvishwa na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ lakini hawakufikia hatua ya kufunga ndoa wakaachana solemba.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.