MICHEZO: Jack Warner Afungiwa Soka Maisha FIFA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MICHEZO: Jack Warner Afungiwa Soka Maisha FIFA

Jack Warber akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani Port of Spain siku ya Alhamisi
Jack Warner akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani Port of Spain siku ya Alhamisi
Makamu wa rais wa zamani FIFA Jack Warner amefungiwa kushiriki soka maisha.
Raia huyo wa Trinidad, 72, ni kiongozi wa zamani wa Shirikisho la soka la Caribbean na Amerika ya Kaskazini na Kati (CONCACAF), lakini alijiuzulu Fifa mwaka 2011.
Anapambana na kusafirishwa kwenda Marekani kukabiliana na mashtaka ya rushwa na anakataa mamilioni ya dola ya rushwa.
Warner alikubali, “vitendo vingi na vya tofauti vimeendelea kujirudia” lilisema shirikisho hilo la soka.
Makamu wa rais wa zamani wa FIFA Jack Warner
Makamu wa rais wa zamani wa FIFA Jack Warner
Sheria za FIFA zinatumika kuchunguza mchakato wa kuhodhi Kombe la Dunia 2018 na 2022, ambazo zilianza kuchunguza vitendo vya Warner tangu Januari 2011.
Siku ya Jumanne, FIFA ilisema Warner amekutwa na hatia ya kuvunja maadili ya shirikisho hilo mara kadhaa.
Taarifa inasema hivi: “Katika nafasi yake kama afisa wa soka, alikuwa mtu muhimu katika njama za kukubali ofa, malipo yasiyo halali na hata mbinu za kujipatia fedha kinyume cha sheria.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.