Michezo: Blatter Agoma Kustaafu FIFA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Michezo: Blatter Agoma Kustaafu FIFA

Rais wa FIFA Sepp Blatter
Rais wa FIFA Sepp Blatter
Sepp Blatter ameeleza ataendelea kubaki kama rais wa FIFA pamoja na kufunguliwa mashtaka dhidi yake kwa sababu hajafanya kosa lolote, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanasheria wake.
Blatter pia alisisitiza malipo ya pauni milioni 1.3 kwa rais wa UEFA Michel Platini kwa kazi aliyoifanya kwa miaka tisa iliyopita yalikuwa halali.
Blatter na Platini wote wanachunguzwa na kamati ya maadili ya FIFA kufuatia kufunguliwa kwa kesi dhidi ya rais wa FIFA.
Blatter akiwa na rais wa UEFA Michel Platini
Blatter akiwa na rais wa UEFA Michel Platini
Taarifa kutoka kwa mwanasheria wa Blatter ilisema: “Rais Blatter alizungumza na wanafanyakazi wa FIFA na kuwataarifu kuwa anashirikiana na uongozi, na kusisitiza hakuna kosa alilolifanya na kudai ataendelea kuwa rais wa FIFA.
Mashtaka dhidi ya Blatter yalifunguliwa na mwanasheria mkuu wa Uswisi siku ya Ijumaa na zikiemo haki za Televisheni zilizouzwa na makamu wa rais FIFA Jack Warner pamoja na malipo ya Platini.
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.