Mbasha Sasa Ni Mtu Huru, Ashinda Kesi Ya Ubakaji ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mbasha Sasa Ni Mtu Huru, Ashinda Kesi Ya Ubakaji !

Mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha, ameshinda kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada ya mahakama ya Wilaya ya Ilala kuthibitisha hana hatia.
ema mbasha
Mbasha ambaye ni mume wa Flora Mbasha amesema anashukuru kushinda kesi hiyo iliyokuwa ikimnyima amani.
“Mungu ni mwema sana amenitetea nimeshinda kesi,” Mbasha ameiambia 255 ya Clouds FM kwa furaha kubwa. “Leo ndio ilikuwa hukumu yangu imesomwa, kwahiyo namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kunisaidia kuwa huru na kuachiwa. Nimekutwa sina hatia yoyote, hilo ndio kubwa ambalo nina mshukuru Mungu.”
“Kwa sasa hivi na ninawashukuru watanzania wote kwa kuniombea maana yake nilikuwa kwenye kipindi kigumu sana katika maisha yangu. Nimekuwa na mapito mazito, nimekuwa nachanganyikiwa, ni wakati mgumu sana siwezi nikamweleza mtu akanielewa. Unakuwa una kesi kubwa halafu huelewi mwisho wako utakuwa vipi! Nilikuwa nikijitahidi kuwa na furaha lakini mwisho wa siku nikikumbuka kesi inayonikabili nakuwa mpweke.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.