MASKINI SAUDA MWILIMA AJIFUNGUA MTOTO, AFARIKI DUNIA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MASKINI SAUDA MWILIMA AJIFUNGUA MTOTO, AFARIKI DUNIA

Bet Sasa
 
Mtangazaji mahiri wa Kituo cha Televisheni cha Star TV, Sauda Mwilima akiugulia

Mtangazaji mahiri wa Kituo cha Televisheni cha Star TV, Sauda Mwilima hivi karibuni alipatwa na majonzi mazito baada ya kujifungua mtoto kwa upasuaji ambaye kesho yake alipoteza maisha, akimuacha akiwa hoi kitandani.
Sauda na mumewe, Best Kauli Juma.
Hii ni mara ya pili kwa mtangazaji huyo wa habari za burudani kutokewa na jambo hilo, kwani miaka michache iliyopita aliwahi kujifungua mtoto ambaye naye alifariki. Katika tukio la juzi, mtoto huyo aliyekuwa wa kike, alizaliwa akiwa na umri wa miezi saba.
Akizungumzia tukio hilo, mume wa mtangazaji huyo aitwaye Best Kauli Juma alisema kwa sasa hali ya mkewe inaendelea vyema ingawa bado kalazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Alijifungua Jumatano iliyopita na kesho yake mtoto akafariki, mimba ya kwanza nayo alijifungua mtoto wa kiume lakini haikuwa bahati, tumeumia ila tunamshukuru Mungu kwa kuwa mke wangu hajambo,” alisema Best.

Chanzo-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.