Magufuli Kurudishia Ardhi Iliyoporwa ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Magufuli Kurudishia Ardhi Iliyoporwa !

Bet Sasa
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli amewaahidi Watanzania kuwa baada ya uchaguzi mkuu na kufanikiwa kuwa rais atarudisha ardhi yote iliyoporwa na  baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na  vigogo wa serikali ambao wameshindwa kuiendeleza.


Dk Magufuli alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa eneo la Mtimbila, Kilombero na Ifakara ambapo alisema kuwa anatambua changamoto ya ardhi ambayo imesababisha upendo kuanza kupotea na anataka kuirudisha kwa kutenda haki ya matumizi ya ardhi.

Alisema kuna ardhi kubwa inayomilikiwa na baadhi ya vigogo wa serikali na wafanyabiashara, hivyo atatumia sheria namba nne ya ardhi kumwezesha kurudisha ardhi hiyo kwa wananchi ili waitumie kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

"Nitarudisha ardhi ambayo inamilikiwa na wafabiashara na vigogo ambao wameshindwa kuiendeleza,hatuwezi kuacha wananchi wanateseka wakati kuna ardhi ya kutosha," alisema Dk.Magufuli.

Aliahidi kuwa atakapokuwa Rais atasimamia hilo kwa nguvu zake zote na kuongeza hatashindwa kururdisha ardhi na mashamba makubwa yanayomilikiwa na watu wachache.

Alisema mbali ya kurudisha ardhi inayomilikiwa na wachache atatumia nafasi kuongeza matumizi ya ardhi kutoka kwenye mapori ya serikali hadi kumilikiwa na wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Mtimbila, alisema anatambua kuwa wananchi wa eneo hilo wana mgogoro mkubwa wa ardhi na hivyo atautafutia ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kurudisha kwa wananchi mashamba makubwa.

Wakati huo huo,  aliwataka wakulima na wafugaji kuishi kwa amani na utulivu na hiyo ndio Tanzania anayoitaka na nchi ikiwa na amani maendeleo yatapatikana.

Aidha, aliahidi kushirikiana na marais waliostaaafu kuamua mambo ya msingi.

Alisema sifa kubwa ya Tanzania ni kuwa viongozi wastaafu wengi wakimo marais ambao wametangulia kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na ya nne.

“Iwapo nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza . Yupo Mzee Ali Hassan Mwinyi, wa awamu ya pili, Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete, na  Salimn Amour pampja na mstaafu Amani Abeid Karume.


CHANZO: NIPASHE

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.