Magufuli Akabidhiwa Msumeno Wa Kuwakatia Mafisadi Nchini. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Magufuli Akabidhiwa Msumeno Wa Kuwakatia Mafisadi Nchini.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli (katikati) akishangiliwa na wananchi wenye ujumbe wa kumuunga mkono  huku akiwa na mfano wa msumeno wa kuwakatia wezi na mafisadi  akishinda urais wakati wa mkutano wa kampeni  mjini Igunga , Tabora jana.
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Maswa ili achaguliwe kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
Mgombea ubunge Jimbo la Maswa kupitia CCM,Stanslaus Nyongo akijinadi kwa wananchi kwenye Uwanja wa Mpira mjini Maswa ambapo pia D.k Magufuli alifanya kampeni.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdalah Bulembo akielezea wasifu mzuri wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli na kuwaomba wananchi kumpgia kura nyingi ili ashinde urais.
 Wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mjini maswa.
 Dk Magufuli akizungumza na wananchi wakati akijinadi  mjini Malampaka, Maswa, ambapo alisema akishinda urais ataanzisha viwanda vingi ili kuongeza thamani ya mazao nchini
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi msafara wake ulipozuiwa na wananchi katika Mji wa Mwigumbi wilayani Kishapu Mwanza
 Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwigumbi  Kishapu mkoani Shinyanga
 Dk Magufuli akihutubia wananchi katika Mji wa Maganzo mkoani Shinyanga, ambapo aliomba kumpigia kura ali ashinde awasaidie kuboresha sekta ya uchimbaji madini kwa serikali kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo  kwa kuwapatia mitaji  na vifaa.
 Mfanyabiashara akiwa amebandika mabango ya kampeni za Dk Magufuli na mgombea ubunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi.
 Kikundi cha vichekesho cha Futuhi kikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kishapu jana.
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akijinadi na kuelezea jinsi serikali ya CCM itakavyoboresha sekta mbalimbali nchini.
 Wasanii wakimsikiliza Dk Magufuli akijinadi mjini Kishapu.
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika  Kijiji cha Igurubi wilayani Magu jana.
 Sehemu ya umati wa wanaachi katika mkutano wa kampeni za Dk Magufuli mjini Igunga
 Dk Magufuli nakiwa na mfano wa msumeno aliopewa na wananchi ili utumike kuwakatakata mafisadi na wabadhilifu wa mali za umma.
Sehemu ya umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM wilayani Igunga.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.