Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) yamewasili Bandarini Dar es Salaam - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) yamewasili Bandarini Dar es Salaam

TATIZO la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua kufuatia kuanza kupindi cha mpito cha mabasi Yaendayo Haraka (BRT) mwezi ujao kufuatia kuwasili kwa mabasi 138 katika Bandari ya Dar es Salaam kutoa China tayari kwa huduma ya usafiri. 
Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki aliwaambia waandishi wa habari jana wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa mabasi hayo, kuwa wakazi wa Dar es Salaama kwa sasa wataanza kutumia usafiri wa mabasi hayo. 
“Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito," hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili", alisema na kuongezeas kuwa kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo tangazwa itasaidia wao kushindana. 
Alisema serikali ilifanya kazi kubwa kuwainganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDA-RT. 
Aidha alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Tsh. 900 zilizotolewa katika mitandao ya jamii, na kusema huo ni uzushi na upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo.
Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia. 
Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit(UDA-RT),Bw,Subri Maburuki alisema mabasi yote yameingia yakiwemo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya kukamlisha taratibu za bandari. 
“Tuliahidi kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni keli yamemekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa jumla mabasi 140", alisema Bw. Maburuki na kufafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama walivyokubaliana. 
Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alisema meli iliyobeba mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi ilitokea China ilikuwa imebeba magari 1700 yakiwemo mabasi ya UDA-RT.
“Hatua hii ni ya msingi kwa nchi yetu, itasaidia wakazi kusafiri kwa urahisi na haraka,”alisema Bw. Mhanga.UDA-RT ni kampuni iliyoundwa na wazalendo kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya DART jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki (kulia) akiwa katika bandari ya Dar es Salaam alipofanya ziara ya kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) tayari kuanza kwa kuanza huduma ya kipindi cha mpito mwezi ujao. Kushoto ni Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni UDA Rapid Transit (UDA-RT),Bw. Robert Kisena ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wa pili kushoto ni Msemaji wa Kampuni hiyo,Bw, Sabri Maburuki.


Sehemu ya mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT)kuanzaia mwezi ujao

Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha mpito

Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mpito.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.