Lulu Afungukia Siasa na Kura Yake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Afungukia Siasa na Kura Yake

Okay....nimeulizwa na Wengi na pengine yanasemwa mengi kuhusu ni Chama kipi cha Siasa nina support Kama ilivyoonekana Kwa Wasanii Wenzangu wengine..! Kwa kifupi nitajaribu kufafanua machache Kwa huu uwezo mdogo wa kufikiri nilijaaliwa na Mwenyezi Mungu..!

Kwanza,kila binadamu/mwananchi ana uhuru wa kuchagua na ku support anachokipenda...kwahyo sitangaa wala kuchukia Flani ku support upande flani


Pili,Mimi Kama mm(binafsi)hii ni Mara yangu ya kwanza kupiga kura kwahyo nimeamua kuitumia Kwa busara na kuifanya iwe na kwanza isiyo na majuto Kwa kutofuata mkumbo wowote wa ndugu,jamaa,marafiki au watu walionizunguka..!

Tatu,Nimependa kuitumia NAFASI hii zaidi Kwa UHUSIKA wa ELIZABETH na sio LULU nikimaanisha ikiwa kila kura ya mwananchi wa wakawaida ni ya siri na kuuridhisha moyo wake basi na mm nitakuwa mwananchi wa kawaida kbsa katika hili..!

Nne,natoa pongezi Kwa wasanii wenzangu waloweza kushiriki Kwa namna moja au nyingine ktk ku support upande mmoja au mwingine kwani wameonyesha ujasiri na mapenzi ya kweli Kwa vyama wanavyo support ILA tu mabishano ya HOJA ni mazuri zaidi na yanaweza kuepusha ugomvi au kuvunja mahusiano yetu ambayo yalikuwepo kabla ya UCHAGUZI na yatatakiwa kuendelea kuwepo baada ya UCHAGUZI..!

Tano,Nawatakia Kila La kheri Wagombea wote na Natumaini Uchaguzi utakuwa wa SAWA na HAKI..! Mwisho,mimi nimejiandikisha na nina KIKATIO changu 
tayari,napenda kuwahimiza wananchi/WaTanzania wenzangu kujitokeza katika uchaguzi ili kumchagua yule unayeona anakufaa....tuombe Mungu na Tujitahidi uchaguzi uwe wa Amani na tuepuke maneno au vitu Vyovyote vinavyoweza kuashiria kuleta vurugu katika uchaguzi wetu Mkuu...!

MunguIbarikiTanzania
KuelekeaUchaguziMkuuOctober2015
KuraYanguSiriYangu

Elizabeth Michael ‘Lulu’ “elizabethmichaelofficial” on Instagram

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.